top of page

SIKU YA WAFAMASIA DUNIANI, SERIKALI YATAKIWA KUANGALIA AJIRA ZA WAFAMASIA

PST Day.jpg

Na Mwandishi Wetu, 
 
Licha ya Tanzania kukabiliwa na uhaba wa watumishi wa Afya katika vituo vya kutoa huduma za Afya nchini, imebainika kuwa bado kuna wafamasia wanamaliza katika vyuo mbalimbali hapa nchini nan je ya nchi wako mtaani hawajapata ajira mpaka sasa. Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es salaam na Rais wa chama cha Wafamasia nchini (PST), Fadhil Hezekiah wakati wa maazimisho ya awali ya siku ya wanafamasia Duniani .

Hezekiah, amesema shirika la afya Duniani (WHO) limeeleza kuwa kuna idadi ndogo sana ya watoa huduma wa Afya ukilinganisha na wagonjwa wanao wahudumia kwa bara la Africa ambalo Tanzania ni miongoni mwa nchi za bara hili. Aidha, Hezekiah ametoa rai kwa serikali na kuitaka kutupia jicho changamoto ya wafamasia kukosa kazi kwa kuwaajiri na kuwapeleka kwenye vituo vya afya wakatoe huduma ili kutatua changamoto hiyo.

Hata hivyo, Hezekiah amesema wakati dunia ikiadhimisha siku ya wafamasia, bado Dunia inashuhudia ongezeko kubwa la usugu wa Dawa, Ongezeko la matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktarin a ongezeka la watu kutumia Dawa bila kupima. Katika hatua nyingine, amewataka watanzania kuacha kutumia dawa bila kufuata ushauri wa Daktari kwa sababu hiyo inapelekea magonjwa mengi kuwa na usugu wa dawa zenyewe.


 
Mwisho.
 

bottom of page